Imaam mmoja nchini rwanda afungwa jela kwa kumuua nguruwe msikitini


Mahakama moja mashariki mwa Rwanda imemhukumu Imam mmoja kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kuua nguruwe msikitini.

-

Mashahidi waliambia mahakama kwamba waliona Bw Musengimana "akimpiga kwa nguvu nguruwe huyo kwa kipande kikubwa cha mbao" na kumuua papo hapo, waraka ulioonekana na BBC unasema.

-

Yusuf Nsengiyumva, wakili wa Bw Musengimana, analaani "hukumu kali" kwa mteja wake akisema alimuua mnyama huyo kwa bahati mbaya.

0 Comments