Kundi la Dola la Kiislamu ladai kuhusika na mauaji msikitini Kabul


Kundi lijiitalo Dola la Kiislamu limedai kuhusika na mashambulizi kwenye msikiti mmoja kwenye mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, siku moja baada ya waumini 10 kuuawa kwenye mashambulizi hayo.


 Kupitia ujumbe wake wa Telegram, kundi hilo limesema lilitega bomu kwenye basi karibu na eneo liitwalo Sekta 6 mjini Kabul. 


Kundi hilo lilitowa idadi hiyo hiyo ya watu kumi waliouawa, sawa na waliotolewa na wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan. Polisi mjini Kabul wanasema watu wengine 30 walijeruhiwa kwenye mashambulizi hayo ya siku ya Ijumaa. 


Maafisa wa Afghanistan wanasema mashambulizi hayo yaliwalenga waumini wa madhehebu ya wachache ya Sufi, ambao walikuwa wakiendelea na tasbihi zao baada ya kumalizika kwa sala ya Ijumaa. Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, alitowa taarifa ya kulaani mashambulizi hayo jana Jumamosi.

0 Comments