Rais mwinyi ahutubia baraza la iyd ukumbi wa abdulwakil kikwajuni unguja jijini zanzibar

 


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akifuatilia tafsiri ya maelezo mafupi ya Aya Suratul-Fat’hi wakati wa hafla ya Baraza la Eid Fitry lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Unguja na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman.(Picha na Ikulu)


BAADHI ya Mawaziri na Wageni waalikwa katika hafla ya Baraza la Eid Fitry wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akilihutubia katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Unguja Jijini Zanzibar leo 3-5-2022.(Picha na Ikulu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akipokea salamu ya heshima kutoka Kikosi cha Jeshi la Polisi cha FFU gwaride maalumu lilioandaliwa kwa ajili ya Baraza la Eid Fitry katika viwanja vya ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Unguja Jijini Zanzibar leo 3-5-2022.(Picha na Ikulu)

0 Comments